Pages

Saturday 12 October 2013

VIDEO YA KIMUGINA YA LINEX KUZINDULIWA WEEK IJAYO:

Mwimbaji nyota wa Bongo fleva,Linex ametangaza kukamilika kwa video ya wimbo wake mpya wa Kimugina.
video hiyo ilitengenezwa chini ya director Adam juma wa visual lab.
na mwanadada atakayeonekana ndani ya video hiyo ni mrembo Jck cliff aliyewahi tesa kwenye video ya Ngwair,she got gwan na nataka kulewa ya Diamond.
Video inatarajiwa kuzinduliwa week ijayo kwenye ukumbi wa Amassadors lounge jijin Dar es salaam.
akisindikizwa na Chid benz,Recho,Amin na Barnaba pamoja na Stara Thomas.
creadit teamTZ
TOA MAONI YAKO HAPA:

WAKAAZI:VIDEO YA TOUCH IKO TAYARI THE VIDEO IS NICE:

Rapper mwenye uwezo mkubwa wa kutumia lugha mbili ‘bilingual’ Webiro N. Wasira maarufu kama Wakazi amesema video ya wimbo wake ‘Touch’ iko tayari na anajiandaa kuiachia ili watu waweze kuiona akianza na watu wake wa karibu na wadau wa media.
Wakazi amefunguka katika kipindi cha ‘The Chat’ cha 100.5 Timesfm kinachoendeshwa na Ezden Jumanne a.k.a Ezden The Rocker jumamosi saa nne kamili asubuhi hadi sita kamili mchana.
“Ebana video ya Touch iko tayari na maandalilzi yako fresh, editing na kila kitu kimeshafanyika so kilichobaki hapa sasa hivi naandaa just like planning kuhakikisha kwamba nairelease proper watu waweze kuiona ili. Mostly watakuwa watu wa media, watu wa radio, television, watu wa newspapers na blogers na watu wengine wa karibu waweze kuiangalia halafu baada ya hapo tutaiweka online and then tutaipeka kwenye different media as well,  kuhakikisha tunai-premier huko pia.”
Wakazi ameielezea kwa ufupi video yake kuwa ni video nzuri na kwamba kazi waliyoifanya ni kubwa na kwamba hatawaangusha fans wake. “ The video is nice and I’m happy kwa sababu tulifanya kazi ya ziada and the song is doing well and shout out to Timesfm kupitia ‘The Chat’, na watu wote wanaousikiliza wimbo na kuupenda pia.
(picha/habari Timesfm)
TOA MAONI YAKO HAPA:

Thursday 10 October 2013

(NEW VIDEO ZANZIBAR)NASSIR VANILLA - SI UTULIE



TOA MAONI YAKO HAPA:

Exclusive;GOSBY ACHAGULIWA KUPERFOM COST 2 COST MAREKANI:

 Via Times Fm;
Rapper Gosby toka B Hits ambae wimbo wake ‘BMS’ umechaguliwa kuingia kwenye mixtape maarufu duniani ya Coast 2 Coast afunguka exclusively kupitia tovuti ya Timesfm kuwa tayari amechaguliwa rasmi kuperform kwenye concert ya Coast 2 Coast San Antonio Edition, lakini hataweza kuhudhuria.
“Jamaa wamenitumia Email juzi usiku kwamba nimechaguliwa kuperform pale San Antonio, wakanitumia na maelezo mengine, jinsi ya kufika, tarehe ya kufika, sehemu ya kufika na nikifika nimuone nani pale kwa sababu jamaa wako professional sana, lakini bado sijawajibu kwa sababu walisema kama kuna chochote ambacho sijakielewa naweza kuwasiliana, lakini niwe mkweli tu na sitaki kudanganya watu kwa sababu hivi vitu vinaenda mbali ujue,  sitaenda na sifikirii kwenda kwa kweli.” Amesema Gosby.
Rapper huyo ambae jana ameachia wimbo wake mpya ‘Monifere’ aliowashirikisha Vanessa Mdee ameelezea sababu zinazosababisha ashindwe kwenda jijini San Antonio.
“Kwa sababu imekuja wakati ambao sio mzuri sana kwangu kwa sababu kuna vitu ninavyofanya, mfano sasa hivi nimeachia ngoma au sio..natakiwa kuhakikisha naisambaza vizuri na naipromote inawafikia watu wote, nahitaji muda mwingi kwa kweli, nataka kujua nafanya video gani vile. Na ndo maana nimesema imekuja kipindi kibaya kwa sababu sifikirii yani hata ingetokea deal ya shilling ngapi mtu aniambie ooh nakupa deal twende sehemu flani siwezi kufanya kwa sababu najua hiki nachokifanya kinaweza kunipa hela hata zaidi ya hiyo ya huko ambako ningeweza kwenda.” Amefunguka mfalme wa Swaghili flow.
TOA MAONI YAKO HAPA:

Friday 4 October 2013

LINA AMEFUNGUA KAMPUNI YA MAVAZI ''NEYONCE DISGNER''


Akizumgumza na Bongo5 leo akiwa mkoni Tanga kwaajili ya Serengeti Fiesta, Linah amesema kampuni hiyo ambayo imeshaanza kufanya kazi jijini Dar es salaam, tayari imeajiri vijana wawili na ina ofisi ya kudumu pamoja na mashine mbalimbali za shughuli za ushonaji.
“Tumefungua kampuni ya mavazi ambayo nimeshirikiana na binamu yangu ,itakuwa inajihusisha na shughuli za ubunifu wa mavazi mbalimbali, ushonaji pamoja na mambo mengine na lengo letu kuwa na kampuni kubwa ya ushonaji ambayo itakuwa na brand kubwa inayotambulika Tanzania nzima,” alisema Linah.
“Nataka kuacha na dhana ya kutegemea muziki peke yake kwasababu muziki una mwisho wake, inatakiwa wakati tuna uwezo wa kufungua kampuni ambazo zitatuongezea kipato ni vyema kufungua ili kuwa na uhakika wa vyanzo vingi vya mapato pamoja na kutoa ajira kwa wengine.”
BONGO5.COM