Pages

Sunday 8 September 2013

TUSKER PROJECT FAME (TPF) YASAKA VIPAJI TANZANIA:

Usahili wa kusaka vipaji vya kuimba kupitia mashindano makubwa kabisa ya Tusker Project Fame 2013, unaendelea na siku ya leo Jijini Dar es Salaam pale Makumbusho ya Taifa kuanzia saa 2 kamili asubuhi.

Hii ni nafasi kwa wale wote ambao wana kipaji cha kuimba kutimiza ndoto zao na kufanikiwa kimuziki, na msisimko mkubwa kutoka usahili wa mwaka huu, Ni ushiriki wa Mzee Ally Zahir Zorro kama moja ya majaji.


Vipaji vitakavyopatikana kupitia usahili huu, vitaingia katika mchuano sambamba na washiriki kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki katika Academy ya muziki ya Ruaraka, ambapo mbali na mafunzo ya muziki mashindano, kutakuwa na shughuli mbali mbali za kuburudisha na kusisimua.


Kumbuka kuwa matangazo yote ya mashindano haya yatakuwa yakirushwa kupitia EATV pia kila jumapili, kuanzia saa 2 kamili Usiku.
TOA MAONI YAKO HAPA:

0 comments:

Post a Comment